KWA WANAFUNZI WOTE WANAOJIFUNZA LUGHA YA KISWAHILI KUANZIA---A B C ZA AWALI , SHULE ZA MSINGI , SEKONDARI KUANZIA KIDATO CHA I--VI , WANAFUNZI WA VYUO NA VYUO VIKUU , WAGENI TOKA NCHI MBALIMBALI . DIPLOMA(STASHAHADA), WALIMU WA KISWAHILI-- SEKONDARI NA VYUO . WALIMU WANAFUNZI -VYUO VIKUU .WATAALAMU MBALIMBALI WA FASIHI YA KISWAHILI.
- HOME
- METHALI , MISEMO, UFAFANUZI NA MATUMIZI YAKE
- BUSTANI YA MALENGA
- MBINU NA KANUNI ZA KUSOMA NA KUFAULU MI...
- UTAKUZAJE UWEZO WAKO WA LUGHA ?
- SWAHILI---ENGLISH DICTIONARY
- KISWAHILI { SWAHILI }--AFRICAN LANGUAGES
- SWAHILI DICTIONARY ONLINE TRANSLATION-LEXILOGOS...
- SWAHILI ALPHABET, PRONUNCIATION AND LANGUAGE
- USEFUL SWAHILI WORDS
- SWAHILI TRANSLATION DICTIONARIES
- KAMUSI YA KISWAHILI
Tuesday, 10 September 2019
Monday, 9 September 2019
WASIFU WA SITI BINTI SAAD-----RIWAYA / HADITHI--------BY SHAABAN ROBERT
Siti binti Saad alikuwa mwanamke wa kwanza Zanzibar kusimama jukwaani
na kuimba nyimbo za taarab. Katika kitabu hiki, Shaaban Robert
anaelezea juu ya maisha ya umaskini na hali ya chini aliyoishi msanii
huyu, katika jamii ya Zanzibar iliyokitwa na tabaka za kijamii miaka ya
kwanza ya karne ya ishirini. Licha ya kuwa sura yake ati haikuwa nzuri,
alifikia hali ya juu ya nyota wa uimbaji wa taarabu akapendwa na wapenda
taarabu si Zanzibar tu na Afrika ya Mashariki, lakini pia alipendwa
hadi Misri na India. Kwa wapenzi wa taarab bado ni malkia, sawa na
alivyokuwa Om Kulthum wa Misri.
Siti binti Saad was the first woman Taarab singer in Zanzibar. In
this book Shaaban Robert looks at the background of the singer: poverty
and low birth, in a society riven by class and race in early 20th
century Zanzibar. Despite her so-called bad looks, she became a star
whose voice was recognised and loved by many, not only in Zanzibar and
East Africa, but as far as Egypt and India. She was and remains to
taarab lovers, the equivalent of Egypt’s Om Kulthoum.
Saturday, 7 September 2019
SHAIRI : LOLIONDO KWA BABU
Watu viguu na njia, Wanoenda kwa vishindo
Kiongozi wa kanisa, Siku hizi anaganga
Siku imepambazuka, Naamshwa kwa kelele
Najifunga yangu shuka, Kutazama walo mbele
Tayari washazunguka, Kwa Kasisi Ambakile
Kiongozi wa kanisa, Siku hizi anaganga
Miujiza imefika, Babu yeye keshaota
Wote mloathirika, Anzeni kujikokota
Loliondo mkifika, Mizizi inatokota
Kiongozi wa kanisa, Siku hizi anaganga
Iwapo una nafasi, Usiende mhimbili
Ondoa na wasiwasi, Loliondo kuna dili
Dawa bei ni rahisi, Kikombe ni buku mbili
Kiongozi wa kanisa, Siku hizi anaganga
Kashinda madakitari, Walosoma hadi ng’ambo
Magonjwa yote hatari, Yalokuwepo kitambo
Eti mpaka kisukari, kweli babu ana mambo
Kiongozi wa kanisa, Siku hizi anaganga
Ukimwi unatutisha, Ugonjwa kama adhabu
Waganga wamechemsha, Kutafuta matibabu
Kama mbinu zimekwisha, Kajaribuni kwa babu
Kiongozi wa kanisa, Siku hizi anaganga
Kwa babu kuna vioja, Kabla kutoa tiba
Hutangaza yake hoja, Dawa msije kuiba
Mnapata mara moja, Sio kunywa mkashiba
Kiongozi wa kanisa, Siku hizi anaganga
Wala msifanye pupa, Walokwenda ni umati
Babu dawa akikupa, Kunywa kwa kombe la bati
Usipeleke na chupa, Ukayavunja masharti
Kiongozi wa kanisa, Siku hizi anaganga
Aponya kila madhara, Hili wengi wanakiri
Pengine ni biashara, Katumia muhubiri
Kujitoa ufukara, Ajipe na utajiri
Kiongozi wa kanisa, Siku hizi anaganga
Mara bibi wa tabora, keshaibuka na yake
Kujiona ndio bora, Na yeye afaidike
Watu kweli ni wakora, Jamani tuwajibike
Kiongozi wa kanisa, Siku hizi anaganga
Sijui kama ya kweli, Msije mkasusia
Mi nahisi utapeli, Mbuzi ndani ya gunia
Dawa sijaikubali, Maajabu ya dunia?
Kiongozi wa kanisa, Siku hizi anaganga
Namefika kaditama, Dawa zinanitatiza
Babu ataniandama, Malenga kuniapiza
Ninaogopa lawama, Shairi nimemaliza
Kiongozi wa kanisa, Siku hizi anaganga
HAMZA A. MOHAMMED
Wednesday, 4 September 2019
Sunday, 1 September 2019
Saturday, 31 August 2019
Tuesday, 27 August 2019
Saturday, 24 August 2019
Friday, 23 August 2019
Sunday, 18 August 2019
LUGHA NA UTAMADUNI---NADHARIA YA SAPIR AND WHORF
Mnamo karne ya 20 wanaisimu
mahiri waitwao Edaward Sapir na Benjamin Whorf walitafiti lugha za
Amerindia Amerika kaskazini na kugundua kuwa miundo ya msamiati na ya
kisarufi ya lugha hizi haifanani kabisa na ile ya lugha ya kiingereza na
lugha nyenginezo za Ulaya na Asia. Hivyo wakapendekeza nadharia isemayo
kwamba Lugha hutawala namna ya wazungumzaji wake waionavyo dunia.
Ukichunguza baadhi ya misamiati ya wana lugha fulani utakuta kuwa yapo
maneno pekee yanayowakilisha yale wayaonayo mbele ya macho yao au
mazingira yao tu na kutokuwepo kwa neno kuna maanisha kwamba jambo hilo
halipo ‘machoni’ pao. Sawa na kusema kuwa ‘lisilokuwepo machoni na
moyoni halipo’. Nadharia hiyo ya Sapir- Wholf, inayojulikana kama
nadharia ya Taathira lugha inaunga mkono mawazo ya awali ya Willian von
Humbolt (1767-1835) pale aliposema kuwa ‘lugha ya mtu hutawala mawazo
yake’. Si wote wanaokubaliana moja kwa moja na ule mtazamo kuwa lugha
hufinyanga uoni wetu wa dunia, wao huchukulia kwamba lugha ‘huakisi’
utamaduni wa wazungumzaji wake. Mjadala huu unaendelea na wanafunzi wana
fursa ya kuendelea nao na kuuchambua kwa kufatilia kazi mashuhuri ya
hivi karibuni ya George Lakoff na Mark Johnson (1980) iitwayo Metaphors
We Live By ambayo ina unga mkono mawazo kuwa lugha hutawala uoni wetu wa
mazingira yanayotuzunguuka wanasema kuwa:
Dhana tulizonazo huunda kile tukionacho,
kutuzunguuka na kinachotuhusu. Mfumo wa dhana ndiyo muhimili wa jinsi
tuionavyo dunia yetu ya kila siku.
Nida ( 1986) anasema kuwa, lugha ni
kielelezo cha utamaduni wa wazungumzaji wake na sio muhimili wa uoni
wao. Lugha hufuata jamii na wala si kuingoza jamii hiyo (Nida, 1986:11)
Angalia:
- Lugha ni sauti za nasibu zinazotumiwa na watu katika kuwasiliana miongoni mwao.
- Jamimi ni kundi la watu wanaoishi pamoja na wenye kuhusiana kijamii, kikazi au kiuchumi na yenye kutumia lugha moja kwa ajili ya mawsiliano yao.
- Lugha imefungamana na jamii kiasi kwamba haiwezi kutenganishwa na maisha ya kijamii ya binadamu.
– Lugha ni kielelezo cha mahusiano ya kijamii yaani hueleza jinsi jamii inavyohusiana na mazingira yao halisi na namna wanajamii wanavyohusiana wenyewe kwa wenyewe.
– Lugha hubadilika kulingana na mabadiliko ya kijamii. Pamoja na uhusiano huu baina ya jamii na lugha, hakuna uhusiano wa moja kwa moja baina ya lugha na jamii kwa sababu:
i) Lugha sio lazima iwe ya watu wa jamii ile ile. Mathalani Kiswahili sio lugha ya Waswahili peke yao.
ii) Watu wanaoishi katika nchi sio lazima wawe wa asili ya nchi hiyo, kwa hivyo jina la jamii yao haiwezi kuwiana na lugha wanayoongea.
iii) Lugha moja huwa na vilugha kadha ndani mwake, mathalani lugha ya Kiingereza ina viingereza yaani lahaja kadha, mfano: Kiskochi, Kikoknii, Kilancastar n.k.
iv) Kuna jamii yenye jina tofauti na lugha wanayozungumza, mathalani Marekani hawazungumzi Kimarekani bali Kiingereza, Tanzania kuna Kiswahili na sio Kitanzania
SHAIRI : NAKUENZI KAMABARAGE
SHAIRI : NAKUENZI KAMBARAGE
**********
Siwezi kukukumbuka,
kimya kimya mtukuka,
mwelekezi muafaka,
u wa maana hakika,
ut’endelea tajika,
milele yote milele.
****
Kwa dhati toka moyoni,
ni shahidi Maanani,
Baba ali mhisani,
wa wanyonge niamini,
alikuwa ni makini,
wa haki za binadamu.
****
Nyerere wetu shujaa,
Afrika aliifaa,
wasifa wake wajaa,
yote yote mataifaa,
mengi mema ulifanzaa,
nakuenzi Kambarage.
****
Shukurani Maanani,
kunigea tungo hini,
nikimtaja mwendani,
aliyeko mtimani,
kulla wa bora imani,
amkumbuke Nyerere.
***
Rwaka rwa Kagarama,
Mshairi Mnyarwanda.
**********
Siwezi kukukumbuka,
kimya kimya mtukuka,
mwelekezi muafaka,
u wa maana hakika,
ut’endelea tajika,
milele yote milele.
****
Kwa dhati toka moyoni,
ni shahidi Maanani,
Baba ali mhisani,
wa wanyonge niamini,
alikuwa ni makini,
wa haki za binadamu.
****
Nyerere wetu shujaa,
Afrika aliifaa,
wasifa wake wajaa,
yote yote mataifaa,
mengi mema ulifanzaa,
nakuenzi Kambarage.
****
Shukurani Maanani,
kunigea tungo hini,
nikimtaja mwendani,
aliyeko mtimani,
kulla wa bora imani,
amkumbuke Nyerere.
***
Rwaka rwa Kagarama,
Mshairi Mnyarwanda.
Friday, 22 March 2019
Thursday, 21 March 2019
Monday, 18 March 2019
Subscribe to:
Posts (Atom)