Swali Lengwa muhimu: Unawezaje kutumia michezo ya jadi ili kusaidia ujifunzaji wa lugha?
Maneno muhimu: kutafakari; utafiti; michezo ya jadi; mapokeo; mashairi; nyimbo; kuchunguza
Matokeo ya ujifunzaji
Mwishoni mwa sehemu hii, utakuwa umeweza:
- umetumia michezo ya jadi na ya mahali husika katika kusaidia shughuli za ujifunzaji;
- umewahamasisha wanafunzi na kuongeza ujasiri wao wa kutumia lugha kwa njia ya michezo, nyimbo na mashairi;
- umepanua stadi zako mwenyewe katika kutafakari wajibu na uwezo wako kwa kuchunguza thamani ya michezo katika ujifunzaji.
Utangulizi
Baadhi ya walimu ambao wamefundisha kwa miaka 20 ni kama tu wanakuwa
na uzoevu wa mwaka mmoja tu, ambao unarudiarudia. Hii ni kwa sababu
hawajifunzi tena kwa bidii au hawajiendelezi ili waweze kuwa walimu bora
zaidi.
Walimu wazuri ni wale ambao wanapanga kile wanachotaka kukifanya, na
mara wanapokifanya, wanarekodi kilichotokea, na kujiuliza wenyewe
mafanikio ni yapi na ni wapi panahitaji kuboreshwa. Wanatafakari endapo
wanafunzi wamejifunza chochote, na kama wamejifunza, wamejifunza nini?
Kwa msingi huu wa ‘tafakari’, wanapanga tena kwa ajili ya shughuli
inayofuata. Nyenzo rejea 1: duara la tenda-tafakari huonesha mchakato huu katika muundo wa kielelezo.
Somo la 1
Watoto hawajifunzi tu wakiwa darasani, wanajifunza pia wakiwa
wanacheza. Wanajifunza kutoka kwa wengine, kwa kuangalia kile
wanachokifanya wengine. Hujifunza kwa kuzungumza, kuimba, kwa kukariri
na kwa kushirikishana katika mazungumzo. Unaweza kutumia mchezo ili
kufanya ujifunzaji katika darasa lako uwe wa mafanikio na kuziba uwazi
kati ya kinachotokea darasani na nje ya darasa.
Katika Shughuli 1, wanafunzi wako wanakuwa kama watafiti, na
wanakwenda kwenye uwanja wa michezo (au mahali pengine) ili kurekodi
kile wanachofikiri kuwa wataweza kujifunza pale. Wanaporudi darasani
wanazungumzia kile ambacho wamekigundua: Unaweza kusikiliza mazungumzo
yao ili kuona kile ambacho unafikiri wanafunzi wako wamejifunza uwanjani
hapo.
Uchunguzi kifani ya 1: Mwanafunzi wa miaka sita ajifunza na kufundishaKiswahili
Maria ambaye ana umri wa miaka sita anasoma katika shule ambayo
Kiswahili ni lugha inayotumika darasani, ingawa si lugha yake ya kuzaliwa.
Kila siku kwa muda wa wiki nzima, Maria aliweza kuonekana wakati wa
mapumziko akiwaangalia watoto wengine wakiruka kamba. Hakujiunga, lakini
alisimama karibu ili kuweza kuona na ‘kusikiliza’ wimbo ambao wanafunzi
walikuwa wakiuimba. Siku ya kwanza ya wiki ya pili, Maria alikuwa
kwenye ile sehemu yake ya kawaida hatua chache kutoka eneo la kuchezea,
lakini sasa aliweza kusikika ‘akitoa sauti’ za maneno ya kwenye wimbo.
‘Ruu-ka, ruuu-kia ndani na seeema
Moja-aa mbili-iii, tatuuu,
Ruuu-kia na-a mimi.’
Alirudia maneno haya tena na tena, akijitahidi kuyasema kwa sauti
kubwa, kwa wororo na kwa kutumia mkazo tofauti tofauti kwenye sehemu za
neno. Alirudia wimbo huu mara kadhaa na kisha kuwasikiliza tena
wanafunzi wengine. Alitabasamu, na kuimba tena ule wimbo.Mwishoni
alitafuta kamba na kwenda kwa rafiki yake, Migueli. Aliimba ule wimbo,
mstari kwa mstari, akimfundisha rafikiye huu wimbo. Alitafsiri yale
maneno ya Kiswahili ili rafiki yake aweze kuelewa alichokuwa akijifunza.
Kwa muda mfupi Migueli aliweza kuimba wimbo ule pamoja na Maria.
Shughuli ya 1: Kuchunguza ujifunzaji wa asili
Kabla ya kuanza shughuli hii, soma Nyenzo Rejea 2: Utafiti juu michezo ya jadi katika mtalaa .
Nyenzo rejea hii inaeleza kazi moja ya utafiti na micezo miwili ambayo
walimu waliibuni kama matokeo ya utafiti huo. Kusoma pia Nyenzo Rejea Muhimu: Kufanya utafiti darasani kutasaidia
sana. Zungumza na wanafunzi wako kuhusu ujifunzaji. Je, wanajua kwamba
daima hujifunzia: nyumbani, shuleni, wakati wanapocheza?
Liambie darasa lifanye uchunguzi katika ujifunzaji wa ‘asili’. Swali
lao ni: Ujifunzaji gani unaotokea wakati watoto wanapocheza? Wanafunzi
lazima waandike na kuchora kuhusu ujifunzaji wanaouona kwenye uwanja wa
michezo na baada ya kutoka shule, wakati wanafunzi wengine wanapocheza,
na wanapocheza wao wenyewe.
Wwaambie wanafunzi darasani washirikishane matokeo yao, kwenye
vikundi. Kiambie kila kikundi kioneshe jinsi ya kucheza mchezo mmoja.
Rekodi nyimbo au mikarara/viitikio wanavyoimba wakati wa mchezo, kwenye
tepu, au kwa kuandika.
Waambie wanafunzi kwenye kila kikundi wajadili kile ambacho wanaweza kujifunza kutokana na michezo hii. Andika mawazo yao.
Umejifunza nini kutokana na shughuli hii inayohusu namna michezo inavyoweza kusaidia katika ujifunzaji?
Somo la 2
Aina zote za michezo zinaweza kutumika kwa kujifunzia na unahitaji
kufikiri kiubunifu jinsi ya kuitumia michezo darasani (angalia Shughuli 2).
Inasaidia kama unaweza kushirikiana na wenzako pamoja na rafiki zako,
na pia kushirikiana na wanafunzi wako, katika kubuni mawazo mapya ambayo
yanaweza kufanya ujifunzaji darasani kwako uwe wa kufurahisha na wenye
mafanikio.
Katika sehemu hii, wewe na darasa lako panueni utafiti wenu kwa
kuwauliza wanajumuiya kuhusu michezo waliyokuwa wanaicheza walipokuwa
wadogo.
Uchunguzi kifani ya 2: Michezo na mikarara/viitikio katika kadi za kusoma
Kuna ongezeko la kupenda lugha nyingi za nyongeza katika mitalaa kote
Afrika. Hii ina maana kuna ujifunzaji wa awali unaotumia lugha mama, na
lugha nyingine za nyongeza (bila kuchukua nafasi ya ile lugha mama).
Mtalaa unalenga kuingiza lugha zote ambazo watoto wanazijua wakati wa
masomo yao.
Bwana Maleke mkoani Lindi hutumia shughuli ifuatayo, ambayo
hujumuisha lugha nyingi za nyongeza, pamoja na wanafunzi wake wa darasa
la 5. Humpatia kila mwanafunzi kipande cha kadi. Wanafunzi huchora picha
katika upande mmoja wa kadi. Kwa upande mwingine, huandika nyimbo,
michezo, mikarara/viitikio au mashairi, ambayo wanayapata nyumbani.
Kila siku, wana kipindi cha kusoma ambapo wanafunzi wanasoma (au
wanaimba!) kile kilichoandikwa kwenye zile kadi. Wakati mwingine,
msomaji bora husoma kadi na msomaji anayesoma polepole zaidi. Wakati
mwingine, mzungumzaji wa lugha moja, humsaidia mwanafunzi mwingine
kusoma lugha yake na kuingiza sauti. Wakati mwingine, wanaigiza hayo
mashairi au wanacheza michezo hiyo. Bwana Maleke amegundua jinsi darasa
lake linavyokuwa na furaha na jinsi wanafunzi wanavyoshirikiana vizuri
katika mazungumzo na wanavyochanganyika vizuri zaidi tangu waanze
kufanya hivi.
Shughuli ya 2: Michezo na nyimbo kutoka kwa wanajumuiya ambao ni watu wazima
Waambie wanafunzi wako wamwombe mtu mzima (mzazi, babu/bibi, jirani
n.k.) awafundishe mchezo, wimbo au mkarara ambao walikuwa wakiufurahia
wakati wa utotoni. Wanatakiwa wajue kanuni za maneno na nyenzo zozote
ambazo zinahitajika.
Siku inayofuata, orodhesha michezo na nyimbo ambazo wanafunzi wamezileta toka nyumbani.
Waweke pamoja wanafunzi wanaojifunza mchezo au wimbo wa aina moja. Waambie wajiandae kufundisha darasa mchezo au wimbo huo.
Waambie waandike huo wimbo au huo mkarara au wacheze mchezo wa kwenye kadi.
Darasa litakapomaliza kujifunza mchezo au wimbo huo, jadilianeni kitu
ambacho wanaweza kujifunza kutokana na mchezo au wimbo huo. Andika tini
kama ulivyofanya hapo awali.
Kwa masomo yatakayofuata, wahamasishe wanafunzi wasome magazeti ili
kutafuta nyimbo, michezo, vitendawili na mizaha kama msingi wa kuandika
vitu vyo wenyewe.
Somo la 3
‘Kuakisi’ ni kutafakari juu ya kile kilichotokea na kuona jinsi ya
kufanya vizuri zaidi wakati mwingine. Baada ya kuwa umejaribu shughuli
mpya, inasaidia sana kuakisi/kutafakari juu ya mafanikio na kitu gani
kinahitaji maboresho. Fanya mchakato wa ‘Panga-Tenda-Rekodi-Tafakari’
kuwa sehemu ya mazoea yako ya kila siku (angalia Nyenzo Rejea 1 ).
Sasa una mkusanyiko mzuri wa michezo, unaweza kuitumia michezo hii
kama msingi wa shughuli za ujifunzaji, na kama msingi wa
kuakisi/kutafakari na uboreshaji. (kazi hii pia inaweza kufanywa kwa
kutumia hadithi.)
Nyenzo Rejea 3: Michezo ya maneno ina michezo kadhaa ambayo unaweza kuijaribu pamoja na wanafunzi wako.
Uchunguzi kifani ya 3: Vitenzi vya Kiswahili katika wimbo wa kurukaruka maneno
Bi Alison aliimba wimbo wa kurukaruka maneno wakati alipokuwa mtoto
pale Mazimbu, Morogoro. Aliamua kuutumia wimbo huo kufundishia wanafunzi
wake wa darasa la 2 maneno kadhaa na virai vya wakati uliopo vya
Kiswahili.
Kwanza wanafunzi waliuimba kwa Kiswahili na kisha aliwasaidia kuuimba kwa Kiingereza.
Alimpatia kila mwanafunzi kipande cha karatasi chenye kitenzi (m.f.
la, nywa, cheka, kohoa, ruka, kimbia, rukaruka) kilichoandikwa kwenye
karatasi hiyo. Alihakikisha kuwa kila mtoto anafahamu maana ya neno hilo
na jinsi ya kufanya vitendo vinavohusiana na neno hilo.
Alimwambia kila mwanafunzi mmoja mmoja afanye vitendo bila maneno, na
darasa liliimba ubeti mpya: ‘Antoni, msichana huyu anafanya nini?
Antoni, msichana anacheka,’ n.k.
Baada ya somo, alitafakari kuhusu:
Kile kilichokwenda vema;
Kile ambacho hakikwenda vema sana;
Kile kilichomshangaza;
Kile ambacho angekibadili kama angerudia lile somo.
Bi Alison alishangazwa na jinsi wanafunzi walivyoutumia muda katika
kujifunza toleo la Kiswahili lakini pia jinsi wanafunzi waliufurahia
muda. Aliona kuwa alihitaji kutumia muda zaidi katika shughuli hii, na
pia kufundisha maneno machache zaidi.
Wiki iliyofuata, alitumia toleo la aina nyingine la Kiswahili
lililokuwa na wimbo wa kurukaruka maneno kwa jinsi ile ile, ya kutunga
beti zenye aina mbalimbali za vyakula.
(Angalia Nyenzo Rejea 4: Wimbo wa kurukaruka maneno kutoka katika wimbo wa kurukaruka maneno wa Igbo.)
Shughuli muhimu: Kujifunza kutokana na mkarara, wimbo au mchezo
Je, kuna mkarara kwenye makusanyo ya darasa lako ambao lugha yake
inaweza kubadilishwa na kuwa kama lugha ya nyongeza na kuweza kutumiwa
katika kuhamasisha ujifunzaji wa lugha?
Bainisha sentensi katika mkarara ambayo neno (au maneno) yangeweza
kubadilishana nafasi kwa zamu. Kwa mfano, ‘Anacheka’ lingeweza
kubadilishana nafasi na (Anaruka, anarukaruka, anakimbia’ n.k.). Kila
mwanafunzi, au kikundi, kinaweza baadaye kuimba ubeti mpya, wenye neno
jipya katika sentensi ya mwanzo.
Ingeweza hata kufurahisha zaidi kama maneno au sentensi yataweza kuambatana na vitendo.
Panga jinsi utakavyopanga darasa lako kwa ajili ya kuimba/ kukariri
na kuigiza (zoezi hili ni mbadala’. (Huu ni mfululizo wa sentensi,
ambazo zinafanana isipokuwa kwa neno au kishazi kimoja. Sentensi hizi
zinatumika kufanya mazoezi ya mitindo ya lugha.)
Kama hutafanikiwa, utatakiwa kujaribu wimbo mwingine, au njia nyingine ya kuendesha shughuli hii.
Nyenzo-rejea ya 1: Duara la tenda – tafakari
Nyenzo-rejea ya mwalimu kwa ajili ya kupanga au kutohoa na kutumia na wanafunzi.
Mpendwa …………………
Darasa letu la …… linajifunza kuhusu hadithi za asili na stadi za
kusimulia hadithi. Tumesikia kuhusu ubingwa wako na tunapenda
kukukaribisha kuja na kutusaidia kujifunza ni namna gani tunaweza kukuza
stadi zetu za kusimulia na kujifunza hadithi pia.
Tungependa uje …………………………………. Tafadhali tujulishe kama muda huu ni
mwafaka kwako. ………………………………… kutoka katika darasa letu atakusubiri geti
la shule saa 4.00 asubuhi.
Tunashukuru sana
Darasa la 5
Shule ya Msingi ya Mtakatifu Maria
Nyenzo-rejea ya 2: Tathmini uigizaji wa hadithi za vikundi
Usuli/welewa wa somo wa mwalimu
Kielelezo kinaonesha hatua zifuatazo katika mduara wa tenda- Akisi/Tafakari:
Panga shughuli.
Tenda kwa kuweka mpango katika vitendo, na chunguza unavyoendelea.
Rekodi kile unachokiona.
Akisi/Tafakari juu ya kilichotokea.
Pitia tena mpango wako, au andaa mpango mpya.
Weka mpango uliopitiwa tena au mpango mpya katika vitendo, na angalia tena.
Rekodi na tafakari tena.
Na kadhalika, na kadhalika …
Kila kitu unachokifanya kama mwalimu kinaweza kuwa sehemu ya mduara wa
Tenda -Tafakari.
(Angalia pia Nyenzo Rejea Muhimu: Kufanya utafiti darasani)
Nyenzo rejea 3: Utafiti juu ya michezo ya jadi katika mtalaa
Usuli/welewa wa somo wa mwalimu
Nonhlanhla Shange alifanya utafiti katika Shahada yake ya Uzamili
katika Kitengo cha Usomeshaji wa Vijijini cha Nelson Mandela katika Chuo
Kikuu cha Fort Hare nchini Afrika Kusini. Alitafiti kuhusu utumizi wa
michezo ya jadi darasani, utafiti ambao aliufanya katika shule nne za
vijijini.
Wanafunzi na walimu wao walifanya utafiti wa vitendo katika michezo ya jadi.
Walimu walisikiliza kwa makini na waliandika tini za michezo ambayo
wanafunzi waliileta darasani. Walijaribu kutayarisha masomo yanayohusu
michezo hii. Wanatunza juzuu, ambamo huwekwa kumbukumbu za masomo haya,
na kujaribu kufanya maboresho kwa ajili ya matumizi ya baadaye.
Maelezo ya michezo miwili ambayo ilichezwa kama sehemu ya utafiti huu ni haya yafuatayo hapa chini.
1. Mchezo wa duara
Matayarisho ya mchezo huu yanajumuisha uchoraji wa kielelezo kama hiki hapa chini ambacho huchorwa ardhini.

Mchezo unachezwaje?
Mchezo huu unachezwa kwa vikundi vidogo vya wanafunzi watano watano
au sita sita. Mwanafunzi mmoja anarukia ndani ya nafasi za duara,
akigeuka upande hadi upande, wakati wanafunzi wengine wakiimba wimbo
mfupi au shairi fupi, kwanza kwa lugha ya asili, na kisha kwa Kiswahili.
Shughuli gani za ujifunzaji zilizohusiana na mchezo huu?
Mchezo ulibuniwa ili kuonesha ni jinsi gani kurudia rudia kwa kutumia
lugha ya wanafunzi wenyewe na lugha ya Kiswahili kunavyoweza kusaidia
katika kujifunza. Kwa kutumia wimbo mfupi au shairi, mchezo huu pia
uliweza kutumika katika kuwafundisha wanafunzi kuhesabu.
2. Mcezo wa mawe
Matayarisho kwa ajili ya mchezo hujumuisha uchoraji wa duara chini
ardhini na kuweka idadi fulanii ya mawe kwenye duara hilo. (duara
lisizidi kipenyo cha mita moja.)

Mchezo unachezwaje?
Wanafunzi wanagawanywa katika vikundi vya watano watano au sita sita.
Kila kikundi kinakuwa na duara lake lililochorwa ardhini na kuwekwa
mawe ndani yake.
Mchezaji anarusha jiwe moja juu; kabla halijatua ardhini, lazima wajaribu kuokota mawe mengine ndani ya duara.
Kila mwanafunzi katika kikundi lazima ajipe namba
mwenyewe (chini ya 10). Namba hii ni idadi ya mawe ambayo mchezaji
atajaribu kucheza na kuokota.
Mchezaji mmoja anaingia kwanza. Kama mchezaji huyu ataokota idadi ya
mawe inayotakiwa kutoka kwenye duara, wanasema orodha ya kuzidisha ya
namba hii (kwa mfano, orodha ya 3 ya kuzidisha, wanakomea kwenye 30 –
hii inaweza kuwa ni ya chini kwa wanafunzi wadogo zaidi).
Kama mchezaji atashindwa kuokota idadi inayotakiwa ya mawe kutoka
kwenye duara, watapaswa kuzidisha idadi ya mawe waliyookota kwa idadi ya
mawe ambayo walipaswa kuokota, na kupata jibu sahihi. Kwa mfano, kama
walitakiwa kuokota mawe hadi 5, lakini wakaokota mawe 3 tu, watatoa jibu
sahihi la 5 x 3.
Wachezaji wengine watapima/watajaji endapo wametoa jibu sahihi au jibu ambalo si sahihi.
Shughuli gani za ujifunzaji ambazo zinahusishwa na mchezo huu?
Mchezo huu ulitumiwa ili kuwafanyia wanafunzi mazoezi ya ’ stadi’ za kuzidisha.
Chanzo cha Asilia: Shange, N., Kitengo cha Mfuko wa Nelson Mandela
wa Usomeshaji na Maendeleo ya Vijijini [ utafiti haujachapishwa ]
Nelson Mandela Foundation’s Unit for Rural Schooling and Development
[unpublished research]
Nyenzo rejea 4: Michezo ya maneno
Nyenzo rejea ya mwalimu kwa ajili ya kupanga au kurekebisha ili kutumia na wanafunzi
Michezo hii inaweza kuchezwa kwa kutumia lugha yoyote na kwa umri
wowote, ilimradi tu wanafunzi wanajua vizuri stadi za kusoma na
kuandika.
Mchezo 1: Bingo
Wasomee wanafunzi hadithi wanayoipenda na waambie wachague maneno mawili wanayoyataka.
Mwulize kila mwanafunzi maneno yao na andika maneno muhimu ubaoni ambapo kila mmoja ataweza kuona.
Ligawe darasa katika vikundi vya wanafunzi sita sita na kiambie kila
kikundi kichague maneno 12 kwa ajili ya kikundi chao. Haya yanaweza
kutofautiana kwa kila kikundi.
Kila mwanafunzi atengeneze karatasi ya bingo kwa kuchora mraba mkubwa
uliogawanyika katika miraba midogo tisa (angalia mfano hapa chini).
Mwambie kila mwanafunzi achague maneno yoyote tisa kutoka kwenye
orodha yao ya maneno 12 na kuyanakili katika karatasi yao ya bingo, neno
moja kwa kila mraba. Makaratasi ya wanafunzi yatakuwa tofauti, kwa
sababu wataweza tu kuchagua maneno tisa kati ya maneno 12.
Mwanafunzi mmoja atakuwa na karatasi kuu yenye maneno 12. Watatoa
maneno bila mpangilio maalum. Neno linavyotajwa kila mwanafunzi ambaye
atakuwa na neno hilo katika karatasi ya bingo atatakiwa kulikata. Wa
kwanza kukata maneno yake yote atapiga kelele ‘Bingo’ na atakuwa
ameshinda.
Kiache kila kikundi kicheze tena na kila mwanafunzi apate zamu ya kutaja maneno.
Kama unataka kutumia karatasi ya bingo zaidi ya mara moja, waambie
wanafunzi wazibe maneno hayo kwa mawe au vihesabio wakati wa kutaja
maneno.
Je, wanafunzi walijifunza maneno mapya? Unajuaje?
Orodha ya Sampuli ya maneno kwa ajili ya Bingo:
Ndizi
Maharage
Kabeji
Mihogo
Nazi
Punje za mahindi
Maembe
Mahindi
Machungwa
Mapapai
Mapeasi
Spinachi
Viazi vitamu
Mifano miwili ya kadi za bingo:
Mchezo 2: Maneno yanayohusu supu
Tengeneza orodha ya maneno tisa, mf. sehemu za mwili, vyumba vya
nyumba, au mboga za majani. Weka orodha hii ubaoni (pembeni mwa picha
toa maelekezo ya maneno kama unaweza).
Mpatie kila mwanafunzi kipande cha karatasi cha mraba, herufi moja
kwa kila mraba. Waambie waingize maneno muhimu katika karatasi hiyo
kwenye miraba hiyo, herufi moja kila mraba mmoja. Waambie kuwa maneno
yanaweza kutoka kushoto kwenda kulia, au juu mpaka chini. Waambie
wanafunzi wajaze miraba ya ziada kwa herufi zozote zile za alfabeti.
(Angalia mfano hapa chini).
Kila mwanafunzi akishafanya hivi, kusanya makaratasi yote na
yachanganye. Sasa wagawie wanafunzi makaratasi hayo bila mpangilio
maalum, na waambie wanafunzi wazungushie maneno yote wanayoweza
kuyapata. Kila mwanafunzi anajua lazima maneno yawe tisa. Wa kwanza
kumaliza ndiye mshindi.
Wanafunzi wanaweza baadaye kuchagua somo lao wenyewe au eneo lao
wenyewe na maneno yanayohusu supu kutoka kwenye orodha hii na kumpatia
rafiki acheze.
Mfano wa maneno yanayohusu supu
Maneno ya kutafuta kwenye maneno ya supu
| Mbuzi |
Ngamia |
| Simba |
Twiga |
| Nyoka |
Nyani |
| Chui |
Farasi |
Unaweza kufanya shughuli hii iwe ya kusisimua zaidi kwa kuwauliza
‘Neno gani ambalo LINALOHUSIKA katika supu?’ Unaweza kutumia mchezo huu
kwa maneno mengi mbalimbali na kwa masomo mbalimbali.
Kiolezo wazi kwa ajili ya maneno ya supu ni hiki hapa chini. Unaweza
kuongeza miraba zaidi au kuifanya iwe midogo zaidi ili kufanya mchezo
uwe mgumu zaidi au mrahisi zaidi kutegemeana na umri na uwezo wa
wanafunzi wako.
Nyenzo Rejea 5: Wimbo wa kurukaruka maneno
Nyenzo rejea ya mwalimu kwa ajili ya kupanga au kurekebisha ili kutumia na wanafunzi
Wimbo wa Kiigbo wa kurukaruka maneno
Ikuku buru gi
Zamiriza
Buru gi buru nwa nnegi
Zamiriza
Nwa nnegi idobere na ukwu osisi kporonku
Chọ ya ịhuyi ya (2x)
Tafsiri ya Kiswahili
Acha upepo ukupeperushe
Zamiriza
Ukupeperushe wewe na mdogo wako wa kike
Zamiriza
Yule mdogo wako wa kike yupo chini ya mti wenye matawi yote yenye kivuli
Unamtafuta mdogo wako huyo, huwezi kumpata (x2)