(a) Msimuliaji (fanani); huyu
ni mtendaji wa tukio la kifasihi mbele ya hadhira. Tukio laweza kuwa
kutamba hadithi, kuimba wimbo au kutoa kitendawili au methali. Huyu ni
muhusika anayesana kazi ya fasihi.
(b) Hadhira; hawa ni walengwa wa kazi ya
fasihi ambao husikiliza na kutazama kinachotendwa na fanani. Hadhira
hushiriki kwa namna fulani kwenye kile kinachotendwa iwe ni kuitikia
wimbo au kupiga makofi, kutingisha kichwa au mwili. Hadhira humsaidia
fanani kujitathimini juu ya kile anachokitenda na mbinu ya utendaji
anayoitumia.
(c) Mandhari; hapa ni mahali ambapo
matukio ya kifasihi yanatendekea. Mandhari huweza kuwa uwanjani,
kichakani, chini ya mti mkubwa au mlimani.
(d) Tukio; hili ni tendo au tukio
linalotendwa na fanani kifasihi. Tendo hili laweza kuwa usimuliaji
hadithi, vitendawili, kuimba au kutoa methali. Kwenye fasihi simulizi
kuna falsafa na mantiki ambayo haipaswi kusahauliwa wala kudharauliwa.
Sengo na Kiango (1977) wanasema; fasihi huweza kulinganishwa na mwamvuli
unavyokinga amali za maisha ya watu.
No comments:
Post a Comment